Rebecca Mbembela (UDSM): Biashara mtandaoni inabadirisha maisha ya wasichana

Rebecca Mbembela (UDSM): Biashara mtandaoni inabadirisha maisha ya wasichana

Biashara na matangazo ya karne ya sasa yanategemea sana teknolojia. Tunaishi ulimwengu wa dijitiali hivyo kila kitu hakina budi kufanywa kidijitali.

Unaweza kuwa na biashara yako au kampuni yako inayotoa huduma ama bidhaa imara na uhakika kabisa lakini usipotumia bidii kujitangaza ama kujiweka online, unaweza kuzidiwa na watu ambao huduma zao hazina ubora zaidi yako.

Kujitangaza (au kutafuta masoko) kimtandao ni njia rahisi na isiyo gharama kuwafikia watu wengi zaidi. Ukweli ni kwamba usipofanya matangazo ya biashara yako, yote uyafanyao yataishia kwa watu wachache tu wanaokuzunguka.

Hata hivyo wengine wanafafanua kuwa imeonekana kuwa kampuni zinazofanya biashara kwa mtindo huo wa kujitangaza zinatabia za kukua kwa kasi na kudumisha ukuaji huo kwa muda mrefu zaidi kuliko zile zinazotumia mfumo wa biashara wa kawaida (traditional businesses).

Hadi kufikia 2011, biashara za mtandao zilikaridiwa kufikia kuwa na thamani ya dola bilioni 100 zikiwa zinatengeneza faida kubwa sana. Haikushangaza kumsikia tajiri mkubwa duniani, Bill Gates, anayemiki kampuni ya software za kompyuta akisema kuwa kama ataruhusiwa kuanza upya biashara, atafanya biashara ya mtandao (network marketing).

Kutokana na faida hizo zinamfanya mwanafunzi Rebecca Mbembela kutoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) naye kufunguka namna ambavyo biashara mtandaoni zinavyobadirisha maisha ya wasichana wengi hapa nchini.

Rebecca ambaye anafanya biashara ya kuuza nguo za kike na kiume, urembo (saa, cheni, herein) katika mitandao mbalimbali anasema amefanikiwa kupata fedha za kujikimu kutokana na ufanyaji wa biashara hiyo.

Anasema amekuwa akiposti bidhaa zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii, email hivyo kupata wateja wengi zaidi wa kununua bidhaa zake.

“Mimi ni kijana niliyeona fursa katika mitandao ya kijamii na kuitumia kuposti bidhaa zangu za urembo na nguo ili kuuza na kupata fedha, kiukweli nimetumia vizuri fursa ya uwepo wa mitandao kwa kufanya biashara.

“Niweaombe vijana wenzangu tutumie mitandao hii kutafuta fursa za biashara na kuacha kuangalia mambo yaw au, kufanya umbea au kutumia kwa matumizi yasiyofaa,” amesema

Rebecca ambaye amesomea kozi ya uandishi wa habari anasema biashara ya mitandaoni ikiwezeshwa inaweza kuiinua nchi ya Tanzania na kubadirisha maisha ya watu wengi.

“Tukubali tu teknolojia imeshakuwa na mitandao kwa sasa inashika kasi katika kupeana taarifa, wetu wengi wanaitumia na kama serikali itaweka utaratibu mzuri nakwambia biashara hii itawezesha kuiinua nchi na wananchi wake,” amesema

Anasema wazo la yeye kufanya biashara lilikuja baada ya kujua matumizi sahihi ya mtandao yanaweza kumuingizia kipato huku akiongeza kusema mbali na biashara anapenda masuala ya fashion.

“Napenda biashara hii kwasababu inafanyika mtandaoni, ila moja ya changamoto ni baadhi ya wateja wanapunguza uaminifu kwamba hawataweza kupata bidhaa zao. Pili, gharama ya kulipia matangazo ili kurasha utembelewe na watu wengi zaidi ambao ni wateja,” anasema

Aidha anasema moja ya faida aliyopata kutokana na biashara hiyo ni kujikimu kimaisha bila kumtegemea mtu yoyote ikiwemo kulipa kodi pamoja na kununua chakula.

“Bado pia inanisaidia nafanya savings kwa kucheza mchezo na kutunza benk ili hapo baadae nifungue duka langu ambalo pia nitaendelea kulitangaza katika mitandao,” anasema na kuongeza

“Fursa nyingi ziko mtandaoni ukizingatia matumizi sahihi ya mtandao. Unaweza ukakaa nyumbani ukaingiza pesa kupitia simu yako kwa kufanya biashara. Ni vizuri kujiajiri na kuondoa utegemezi,”amesema

Hata hivyo anasema kitu kingine anachopenda kufanya ni  kutangaza, kuandika makala zinazohusu watoto na wanawake  na kujitolea katika kuisaidia jamii kwa kufanya kazi na NGO's

“Pia nampenda sana Meena Ally, kwasababu ni mwanamke mpambanaji (mwandishi na mjasiriamali) anafanya vizuri pande zote mbili na anahamasisha vijana wengi kujikwamua kimaisha,” anasema

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags