Rayvanny: Mmezoea kutucheka

Rayvanny: Mmezoea kutucheka

Baada ya show yake aliyofanya nchini Albania na kuonekana kukubalika,  mwanamuziki Rayvanny amefunguka kutokana na maneno ya  baadhi ya watu wanaodai kuwa #Rayvanny alialikwa kwenye show ya Albania kwani wasanii kutoka Tanzania huwa hawajazi  kwenye matamasha yao wakiwa nje ya nchi.

 Rayvanny amedai kuwa watu wasikariri kila siku watanzania wataishia kuimba kwenye Bar na kukosa watu, huku akidai kuwa hata wasanii kutoka nje wanaosifiwa kujaza kwenye show mara nyingi huwa hawafanyi show zao wenyewe bali wanaalikwa.

 Hivyo basi Watanzania wanatakiwa kuusukuma muziki ili ufike mbali na sio kuwa na chuki na kuzoea kucheka wasanii wasipojaza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags