Ray C: Roho yangu inasita kurudi Tanzania

Ray C: Roho yangu inasita kurudi Tanzania

Ikiwa ni mwendelezo wa historia ya mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Rehema Chalamila maarufu Ray C kueleza sababu ya kuondoka Tanzania na kuhamia Paris, Ufaransa, sasa ameweka wazi bado hajafikiria kurudi tena nchini Tanzania.

Ray amefunguka kwa kueleza kuwa hana mpango wa kurudi Tanzania.
“Baada ya kuachana na mpenzi wangu nikamwambia kabisa mimi nafikiri nitarudi Tanzania, lakini baadaye nikakaa nikawaza nikasema I don’t think kama nitaweza ku-survive kukaa Tanzania kwa sababu unajua sijui ni kitu gani mpaka leo ukiniambia kurudi Tanzania roho yangu inasita sijui kwa nini ilikuja tu nikapachukia,” alisema.

Utakumbuka wiki iliyopita Ray C aliweka sababu ya kuondoka Tanzania na kuhamia Paris ikiwa ni kutokana na kutokuwa sawa kiafya hivyo baada ya kupitia matatizo makubwa alitamani kupona kiroho na kubidi aondoke kabisa nchini.

“Nilipitia matatizo, mtihani mkubwa sana lakini namshukuru Mungu kwamba niliweza kusimama tena mwaka 2017/18 nikarudi tena studio nikaanza kurekodi, kufanya kazi na kutoa nyimbo lakini bado nilikuwa nahitaji kupona kwenye moyo."

"Unajua unaweza kupona tu physical lakini moyo bado una mambo mengi kwa hiyo nikasema mimi ili nipate amani ya moyo inabidi niondoke kwa sababu tayari nilishaanza kuona watu hawanichukulii serious, sawa nilikuwa nafanya vizuri lakini sikuona ile thamani,” amesema.

Ray C aliwahi kutamba na ngoma kama ‘Uko Wapi’, ‘Mama Ntilie’, ‘Umenikataa’, ‘Touch Me’, ‘Sogea Sogea’ na nyinginezo kibao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags