Ray C awagawa wasanii chipukizi Bongo

Ray C awagawa wasanii chipukizi Bongo

Ikiwa imepita siku moja tangu mwanamuziki wa zamani wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anaishi jijini Paris, Ufaransa Rehema Chalamila ‘Ray C’ kuwataka wasanii wenye umri mdogo Tanzania hasa wa kike kuchangamkia fursa kama anavyofanya mwanamuziki wa Afrika Kusini, Tyla, wasanii wachanga wamemjibu mkongwe huyo kwa mitazamo tofauti.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C alichapisha video ya Tyla akiwa anatumbuiza katika usiku wa Tuzo za BET huku akiambataniasha na ujumbe wa kuwataka wasanii wachanga kuchangamka ili waweze kufika anga za Tyla.

“Wadogo zangu hasa wa kike changamkeni na nyie mfike hizi steji sielewi tatizo nini mbona mnaimba vizuri tu, au Lugha? ama ni nini? Mbona Fally haimbi kingereza but juzi kati kajaza Arena hapa France, ama management ndiyo shida?.

Sema biashara ya muziki ni pasua kichwa sana yani haka kadada (Tyla) single moja tu kashatoboa na Grammy kabeba duh…!, think Management ni kitu muhimu sana kwa msanii uki-relax unaganda hapohapoa” aliandika Ray C

Kutokana na ushauri huo wa Ray C Mwananchi imezungumza na baadhi ya wasanii wachanga na kuzungumzia mtazamo wao katika kuufanyia kazi ushauri wa nguli huyo wa Bongo Fleva.

Akizungumza na Mwananchi mwanamuziki Gabus Juma ‘D Love’ ambaye amewahi kutamba na ngoma ya ‘Pole’ aliyomshirikisha Kusah ameeleza kuwa suala hilo kwake linaweza kuwa changamoto kutokana na kutokuwa na 'Management'.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post