Rashford agoma kuondoka Man United

Rashford agoma kuondoka Man United

Mshambuliaji wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, #MarcusRashford ameripotiwa kuweka wazi mipango yake baada ya kuwepo kwa tetesi za kuondoka katika ‘timu’.

Kwa mujibu wa The Sun News imeeleza kuwa Rashford amedai kugoma kabisa kuondoka Old Trafford kwa msimu ujao na amezungumza na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo Erik ten Hag, akimwambia kwamba atabadilika na kuwa bora zaidi.

Hata hivyo kocha wa Man United #TenHag amekiri kuwa Rashford hana mpango wa kwenda popote bado yupo katika mipango yake ingawa kuwa mchezaji huyo hakufanya vizuri msimu uliyopita.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo hakufanya vizuri msimu uliopita ambapo ameonekana kucheza mechi 43 za mashindano yote, na kufunga mabao manane pekee huku akiandamwa na kesi nyingi za utovu wa nidhamu nje ya uwanja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags