Rapa T.I aponea kwenye tundu la sindano

Rapa T.I aponea kwenye tundu la sindano

Mwananmuziki kutoka Marekani Clifford Joseph Harris ‘T.I’ alikamatwa na polisi katika uwanja wa Ndege wa Atlanta ‘Hartsfield-Jackson’ baada ya utambulisho wake kudaiwa kuwa sio sahihi.

Kwa mujibu wa Tmz msanii huyo alikamatwa kutokana na utambulisho wake kufanana na mwanaume mwingine aitwaye Clifford Harris kutoka Baltimore, Maryland jina lake likifanana na T.I ambapo mwanamume huyo ni mshukiwa wa ukatili kwa wanawake.

T.I. alichukuliwa kutoka katika uwanja wa Ndege huo na kufikishwa katika jela ya ‘Clayton County Jail’ ambapo wakili wa ‘rapa’ huyo Steve Sadow alieleza kuwa alipigiwa simu na Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Clayton, na kuwataka kumuachia mteja wake ndani ya masaa mawili lakini hakimu aligoma kumuachia.

Aidha masaa machache baadaye T.I aliachiwa huru kutokana na kugundulika kuwa mtu aliyekuwa akitafutwa na polisi kuwa sio yeye kwani Clifford Harris anayesakwa inasemekana ana uzani wa pauni 205, lakini T.I. inaripotiwa kuwa na uzani wa pauni 165.

Hii sio mara ya kwanza kwa ‘rapa’ huyo kuhusishwa katika kesi mbalimbali, utakumbuka kuwa katika miaka ya hivi karibuni zaidi ya wanawake 30 wameripotiwa kumshutumu T.I kwa kuwanyanyasa kingono lakini mpaka leo hajawahi kufikishwa katika vyombo vya sheria kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kufanya atiwe nguvuni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags