Rangnick anukia Bayern Munich kuchukua mikoba ya Tuchel

Rangnick anukia Bayern Munich kuchukua mikoba ya Tuchel

Imeripotiwa kuwa Rais wa klabu ya Bayern Munich Harbert Hainer amethibitisha kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United Ralf Rangnick  kwaajili kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel

Inaelezwa kuwa huenda Rangnick akawa kocha mkuu klabuni hapo baada ya kuondoka Tuchel mwishoni mwa msimu huu ambapo ni mwaka moja kabla ya mkataba wake kutamatika.

Rangnic ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Austria, anasifika kwa kuweza kuongoza miradi endelevu ya kiufundi kama kuwa kocha mkuu, Mkufunzi wa makocha au Mkurugenzi wa Ufundi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 pia anasifika kwa falsafa za soka la asili ya Ujerumani na pia alishawahi kuwanoa kwa nyakati tofauti makocha wakubwa wa Ujerumani kama Jurgen Klopp wa Liverpool na Juilien Negelsman wa timu ya Ujerumani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags