Rangi za kucha zinavyoleta muonekano wa kipekee

Rangi za kucha zinavyoleta muonekano wa kipekee

Karibu tena katika ulimwengu wa fashion ili kufahamu yanayohusu urembo na mitindo mbalimbali ya kisasa.
Leo tutazungumzia upakaji wa rangi kwenye kucha ulivyokuwa kwa kiasi kikubwa.

Kwanza kabisa kuna umuhimu mkubwa wa kucha kwa mwanamke, hauwezi kuwa mrembo ukavaa mavazi mazuri na ukashindwa kupamba na kuzifanya kucha zako kuwa na muonekano mzuri wakuvutia.

Rangi za kucha zimekuwa nakshi bora kwa muonekano wa vidole vya mwanamke. Wanawake siku hizi kupaka rangi kwenye kucha mikononi na miguuni imekuwa ni moja ya njia wanayofurahia kuonesha urembo wao.

Siyo kupaka rangi tu, inakupasa ujue jinsi ya kutunza kucha zako ili zivutie muda wote. Lakini siku za hivi karibuni wanaume nao wamekuwa wakifanya urembo huo ambapo awali ulikuwa pambo la wanawake pekee, lakini kutokana na utandawazi mambo yamebadilika sana.
Kwenye bara la Ulaya imekuwa ni fashion ambayo imezoeleka sana kwa wanawake na wanaume hasa watu maarufu kama Chris Brow, Usher Raymond, Kanye West na wengine wengi wamewahi kuonekana na urembo huo.

Pia katika bara la Afrika nchini Nigeria wanaume wamekuwa wakipaka rangi za kucha japo siyo kwa ukubwa kama mwanamuziki Asake ni moja kati ya urembo anaopenda kiufupi watu siku hizi wamekuwa wakienda na wakati wenyewe wanasema ‘mambo ni mengi muda mchache’
Tumepata wasaa wa kuzungumza na mwanamitindo wa urembo wa kucha Davidi maarufu kama Mr Kucha kutokea Mbagala Kijichi amefafanua kuwa urembo huo umekuwa ukichukuliwa serious tofauti na zamani.

Ambapo watu walikuwa bado hawana hamsa ya kutengeneza na kupaka rangi zenye muonekano kama hivi sasa.
“Hii kazi ya kupaka rangi kwenye kucha kwanza ni urembo wenye muonekano mzuri, siku hizi haiwezi ikapita siku bila mwanamke kutia rangi kwenye kucha zake tena mara nyingi hutumia rangi ya jeli ili aweze kukaa nayo muda mrefu bila kutoka”. Anasema Mr Kucha

Pia amezungumzia kuhusu urembo kuingiliwa na wanaume ambapo zamani ilikuwa ni ajabu kumuona mwanaume kapaka rangi kwenye kucha zake lakini kwa sasa ni tofauti.
“Unajua siku hizi mambo ni mengi tunawaona baadhi ya wanaume wanapaka rangi za kucha lakini kwa hapa Tanzania bado haijawa rasmi kumuona mwanaume anaenda saloon kwa ajili ya kupaka rangi japo naamini wapo wanaotamanani ila kwa ajili ya tamaduni zetu haziruhusu hivyo.

Na kama wapo wanaofanya hivyo basi wanafanya kwa siri sana, kuficha kuonekana watu wa tofauti mbele za watu”. Anasema
Mr Kucha amesema hiyo ni moja ya kazi yake kubwa sana inayompatia kipato mjini na kujikimu mahitaji ya familia yake na ndiyo maana anaifanya kwa ufanisi wa hali ya juu ili aweze kuonekana bora kwa wateja wake.

Mwananchi Scoop haikuishia hapo, ikafika mpaka kwa mwanadada aliyefahamika kwa jina la Mastula Masham mkazi wa buza ameeleza kuwa yeye anapendelea kubandika kucha na kupaka rangi, anabadilisha rangi kila baada ya week moja.
“Mimi huwa napenda urembo wa kucha ila kwa vile kucha zangu hazina uwezo wa kukua sana basi naanza kubandika kucha bandia kisha napaka rangi, inanifanya kuwa comfortable kwa muonekano mzuri”. Anasema Mastula

RANGI ZINAZOPENDEZA KWA MTU MWEUSI

1. Cobalt Bluu
Rangi zilizokolea na zinazong'aa huonekana kustaajabisha kwenye ngozi nyeusi, iwe tunazungumzia vipodozi, nguo au kucha basi unakuwa na muonekano angavu na wenye kupendeza.

2. Chocolate Brown
Chocolate brown inapendeza haswa kwa wenye ngozi nyeusi.

3. Kijani kibichi
Hii rangi inakuwa vizuri zaidi kwenye kucha hasa ukimpata mchoraji akakuchora vizuri lazima utapendeza.


4. Grey
Wengi wanapendelea rangi ya kijivu kwa sababu ni rangi ambayo watu wengi inawapendeza na haichagui ngozi ya mtu kwa sababu inakuwa imetulia.

6. Rangi Nyekundu
Katika rangi ambayo inawafaa sana watu ni rangi hii nyekundu, huleta muonekano wa kipekee kutokana na vidole kupendeza nayo haichagui ngozi wala nguo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags