Ramadhani Brothers washinda AGT kwa mara ya kwanza

Ramadhani Brothers washinda AGT kwa mara ya kwanza

Baada ya kupambana kwa miaka kadhaa katika mashindao ya kusaka vipaji yanayofanyika nchini Marekani, na kutofanikiwa kuchukuwa taji lolote, hatimaye waruka sarakasi maarufu kutoka Tanzania, Ibrahim na Fadhili Ramadhani ‘Ramadhani Brothers’ wameibuka washindi kwa mara ya kwanza katika shindano la ‘America’s Got Talet: Fantasy League.

Licha ya kuondoka na taji hilo ‘Ramadhani Brothers’ pia wamenyakuwa kitita cha dola 250,000 ambayo ni zaidi ya tsh 636 milioni na kuingia katika historia ya kuwa Waafrica wa kwanza kuwahi kushinda shindano hilo.

Kufuatiwa na mahojiano yao waliyoyafanya baada ya kunyakuwa taji hilo walieleza kuwa ushindi walioupata una maana kubwa sana kwao kwani wanamipango ya kuboresha sehemu yao ya kufanyia mazoezi na kununua vifaa vya mazoezi kwa ajili ya waruka sarakasi wengine kutoka Tanzania.

Mara ya mwisho 'Ramadhani Brothers',walishindwa kutwaa ubingwa na kuishia top 5 katika mashindao ya kusaka vipaji ya Australia's Got Talent 2022/2023 (AGT).

Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu wameibuka washindi wakiwapiku washindani wengine ambao ni pamoja na Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags