Ramadhani Brothers waja kivingine America’s got talent

Ramadhani Brothers waja kivingine America’s got talent

Wasanii kutoka nchini Tanzania, Ibrahim na Fadi Ramadhani, maarufu kama The Ramadhani Brothers usiku wa kuamkia leo walishangaza watu kwa kitendo chao kinachoitwa ‘Head-to-Head Balancing Act’ katika usaili wao kwenye America’s Got Talent 2023 msimu wa 18.

Jaji Howie Mandel amekiita kitendo hicho kuwa hatari zaidi ambacho amewahi kuona katika America’s Got Talent.

Katika kipande hiki maalum kutoka kwenye kipindi cha tarehe 6 Juni, Ramadhani Brothers wamewavutia karibu kila mtazamaji aliyekuwepo katika jengo la AGT.

Usaili wa msimu wa 18 wa America’s Got Talent unaendelea katika duru ya pili ya msimu mpya ulioanza Mei 30 ambapo maonyesho ya moja kwa moja yanatarajiwa kuanza rasmi Agosti 22.

Aidha ndugu hawa wanatambulika zaidi kwa sanaa yao ya ‘Acrobatic’ na wamewahi shiriki mashindano mbalimnali makubwa kama Australia Got Talent na kufika fainali.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags