Ramadhani Brothers ndani ya mlima kilimanjaro

Ramadhani Brothers ndani ya mlima kilimanjaro

Washindi wa ‘American Got Talent’, The Ramadhan Brothers wametimiza lengo lao la kupanda na kufika kileleni katika Mlima Kilimanjaro wakiwa na Tuzo yao ya ushindi waliyoipata nchini Marekani.

Lengo hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro limetokana na wawili hao kutaka kufika kileleni wakiwa na picha ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kama ishara ya kumuunga Rais Samia katika kampeni ya kutangaza utalii.

Ikumbukwe kuwa usiku wa kuamkia Februari 20, 2024 waruka sarakasi maarufu kutoka Tanzania, Ibrahim na Fadhili Ramadhani ‘Ramadhani Brothers’ waliibuka na ushindi kwa mara ya kwanza katika shindano la ‘America’s Got Talet: Fantasy League.

Licha ya kuondoka na taji hilo ‘Ramadhani Brothers’ pia waliondoka na kitita cha dola 250,000 ikiwa ni zaidi ya tsh 636 milioni na kuingia katika historia ya kuwa Waafrica wa kwanza kuwahi kushinda shindano hilo.

Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu waliibuka washindi wakiwapiku washindani wengine ambao ni pamoja na Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags