Ramadhani Brothers kutua kesho Dar

Ramadhani Brothers kutua kesho Dar

Baada ya kufanya mambo makubwa na kuondoka na taji la America’s Got Talet: Fantasy League waruka sarakasi kutoka nchini Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramadhani maarufu kama ‘Ramadhani Brothers’ wanatarajia kutua siku ya kesho Machi 8, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Hivyo basi Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kupitia Katibu Mtendaji Basata Dkt. Kedmon Mapana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na michezo Gerson Msigwa wamewataka Watanzania, vyombo mbalimbali vya habari, Wasanii na wadau wa Sanaa kujitokeza kwa wingi kuwapokea mashujaa hao majira ya saa 6 mchana katika uwanja wa Julius Nyerere.

Ramadhani Brothers waliibuka washindi kwa mara ya kwanza katika shindano la la ‘America’s Got Talet: Fantasy League, Februari 19, 2024 ambapo walifanikiwa kuondoka na kitita cha dola 250,000 ambayo ni zaidi ya tsh 636 milioni na kuingia katika historia ya kuwa Waafrica wa kwanza kuwahi kushinda shindano hilo.

Mara ya mwisho 'Ramadhani Brothers',walishindwa kutwaa ubingwa na kuishia top 5 katika mashindao ya kusaka vipaji ya Australia's Got Talent 2022/2023 (AGT).

Fadhili na Ibrahim Ramadhani waliibuka washindi wakiwapiku washindani wengine ambao ni pamoja na Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags