Rais Xi Jinping atarajiwa kufanya ziara Saudi Arabia

Rais Xi Jinping atarajiwa kufanya ziara Saudi Arabia

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhan amekiambia kituo cha televisheni cha Al-Arabia kuwa rais wa China Xi Jinping anatarajiwa kufanya ziara katika taifa hilo la ghuba.

Ameyasema hayo leo baada ya mazungumzo na mwenzake wa China Wang Yi, katika mkutano ambao bin Farhan amesema umefanyika katika wakati muhimu.

Aidha, afisa huyo mwandamizi wa Saudi Arabia amesema nchi yake iko katika hatua za mwisho mwisho za maandalizi ya mkutano wa kilele baina ya China na mataifa ya Kiarabu.

Ziara hiyo ya Xi Jinping nchini Saudi Arabia imetangazwa wakati taifa hilo la kifalme likiwa katika mvutano mkubwa na Marekani ambayo ni mshirika wake wa siku nyingi, hususan baada ya shirika la mataifa yanayouza nje mafuta kwa wingi, OPEC+ linaloongozwa na Saudi Arabia kuamua kupunguza viwango vya uzalishaji, licha ya onyo kutoka Marekani.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags