Rais wa UEF aipa onyo ligi kuu Saudi Arabia

Rais wa UEF aipa onyo ligi kuu Saudi Arabia

Baadhi ya timu kutoka ligi kuu nchini Saudi Arabia kusajili wachezaji wengi wanaoelekea kumaliza maisha yao ya soka Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin ametoa tahadhari ya kutorudia makosa waliyoyafanya China kwenye uwekezaji wa soka.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari kuhusiana na ongezeko la wimbi kubwa la wachezaji wanaoelekea nchini Saudi Arabia Rais huyo anasema kuwa

“Hapana, hapana, hapana, nadhani hilo ni kosa kwa soka la Saudi Arabia kwanini hilo ni tatizo kwao? kwa sababu wanapaswa kuwekeza kwenye akademi, walete makocha, na waendeleze wachezaji wao wenyewe” alisema  Aleksander.

Aliendelea kueleza kuwa “Mfumo wa kununua wachezaji ambao wako karibu kumaliza maisha yao ya soka sio mfumo wa kuendeleza soka, China walifanya kosa kama hilo, mara nyingi walileta wachezaji walio karibu kumaliza maisha yao ya soka” alisema  Aleksander.

Ikumbukwe tu hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la wachezaji wanaoelekea nchini humo akiwemo mshindi wa Balon D’or mara tano Christiano Ronaldo, Karim Benzema, Ng’olo kante pamoja na Odion Ighalo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags