Rais wa Peru aondolewa madarakani

Rais wa Peru aondolewa madarakani

Bunge la Peru limemuondoa madarakani Rais Pedro Castillo na nafasi yake kuzibwa na makamo, Dina Boluarte muda mfupi baada ya Castillo kujaribu kulivunja bunge hilo, ikiwa kabla ya zoezi la kumpigia kura ya kumwondoa.   

Ofisi maalumu yenye kuhusika na masuala ya uchunguzi nchini humo ilisema kitendo cha Castillo anaehusishwa na kupoteza udalifu kazini cha kujairibu kulivunja bunge ni sawa na tukio la mapinduzi. 

Walipiga kura za ndio 101 na hapana 6 huku kura 10 zikiwa zimeharibiwa Muda mfupi kabla ya kupigwa kwa kura hizo Castillo alitanga kuweka serikali ya dharura na kutaka duru ya pili ya mkutano wa bunge ya kufanikisha katiba mpya taifa hilo.

Serikali ya Marekani ilisema imeupokea vyema  uteuzi wa Bibi Boluarte kama Rais wa Peru, ambaye tayari ameapishwa na bunge la taifa hilo katika siku ambayo kulishuhudiwa kiongozi wa aliyeondolewa Castillo akitiwa nguvuni.


Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imepongeza umadhubuti wa taasisi za Peru kwa kuhakikisha umadhubuti wa kidemokrasia na itaendelea kuliunga mkono taifa hilo chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Bibi Boluarte, mwanasheria mwenye umri wa miaka 60, atakuwa mwanamke wa kwanza kufikia ngazi ya urais nchini Peru,ikiwa tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Chanzo: RTR and DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post