Rais Samia aivunja bodi ya mawasiliano

Rais Samia aivunja bodi ya mawasiliano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhandisi Othuman Sharif Khatib.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, Novemba 9, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Bodi hilo imevunjwa kuanzia Novemba 7, 2023 lakini haijaeleza sababu za kuvunjwa kwake.

Mhandisi Khatib aliteuliwa Septemba 2022 na Rais Samia kushika wadhifa huo akichukua nafasi Dk Jones Kilembe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Waliokuwa Wajumbe wa Bodi hiyo ni Mhandisi Othman S. Khatib (Mwenyekiti), Khalfan S. Saleh (Makamu Mwenyeki), Mzee S. Mndewa (Mjumbe), Fatuma S. Ikuja (Mjumbe), Abdallah B. Katunzi (Mjumbe) na Rehema J. Khalid (Mjumbe).
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags