Serikali nchini Congo imesema raia 10 wamefariki baada ya chuo kikuu chao kushambuliwa katika mashambulizi ya anga yaliyotokea katika mji mkuu wa nchini Sudan, Khartoum siku ya Jumapili.
Wizara ya mambo ya nchi za nje ilisema imepokea kwa masikitiko makubwa mauaji ya raia hao yaliyotokea katika Chuo kikuu cha kimataifa cha Afrika.
Waziri Christophe Lutundula alisema kuna dalili kwamba mashambulizi hayo ya anga yalifanywa na jeshi la anga kwenye eneo linalokaliwa na wakazi wasio na silaha, wakiwemo raia wa kigeni.
Aidha Christophe alisema serikali inasubiri maafisa wa nchi ya Sudan kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Leave a Reply