R. Kelly amkingia kifua Diddy

R. Kelly amkingia kifua Diddy

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani, R. Kelly ambaye anatumikia kifungo cha miaka 31 gerezani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono, amewaonya wale wote ambao wanamdhihaki ‘rapa’ #PDiddy ambaye anashutumiwa kujihusisha na biashara za ngono.

Kupitia mahojiano yake aliyoyafanya na #Wack100 kwa njia ya simu, R. Kelly amewajia juu wale wote wanaomcheka na kumtukana Diddy huku akiwataka wasifanye hivyo kwani matatizo kama hayo yanaweza kumtokea mtu yoyote na kwa muda wowote.

Hata hivyo amesema kuwa haamini kesi zinazo mkabili Diddy kwa sababu yupo kwenye matatizo kama hayo na anafahamu nini kinafanyika nyuma ya pazia.

Mwaka 2021 R.Kelly alikutwa na hatia katika kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto kulingana na ushahidi uliyofikishwa mahakamani alihukumiwa kifungo cha miaka 31 jela.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags