Questlove aikataa Hit Em Up ya Tupac

Questlove aikataa Hit Em Up ya Tupac

Mwigizaji na mtayarishaji wa muziki Marekani Questlove, amedai kuwa hakuwahi kuwa shabiki wa marehemu mwanamuziki Tupac wala kuikubali ngoma yake iitwayo ‘Hit Em Up’.

Questlove ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye Podicast ya ‘One Song’ ameeleza kuwa japo watu wengi wamekuwa wakivutiwa na ngoma hiyo lakini yeye hakuwahi kuikubali kutokana na kudai kuwa utayarishwaji wake ulikuwa ni mbovu.

Wimbo wa ‘Hit Em Up’ wa Tupac aliuachia mwaka 1996 ukiwa ni kwa ajili kuwachana wasanii wenzake kama marehemu Biggie Smalls, Junior M.A.F.I.A., na Mobb Deep.

Tupac Shakur alifariki Septemba 7, 1996, baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari huko Las Vegas, Nevada.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags