Profesa Jay atuma ujumbe mzito kwa Ndugai

Profesa Jay atuma ujumbe mzito kwa Ndugai

Eeebwana huko mitandao basi story ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai zinaendelea kupambana moto na kuteka hisia za watu mbalimbali.

Unaambiwa aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na msanii wa muziki hapa bongo, Prof Jay ameshea video fupi ya mistari ya ngoma yake ya ‘nang’atuka’ kwenye mtandao wa Instagram ambapo ni ujumbe maalum kwenda kwa Ndugai baada ya kujiuzulu nafasi yake hiyo ya uspika wa Bunge.

Kwenye video hiyo fupi ilizua gumzo katika mitanmdao ya kijamii, Prof Jay ameandika kwamba “TBT ya kibabe ‘Nang’atuka’ special dedication kwa bwana Ndugai,”

Kama mnakumbuka vizuri ngoma ya ‘Nang’atuka’ ilikuwa ni muendelezo wa ngoma ya ‘Ndio mzee’ ambayo Prof Jay alikuwa akiomba kura kwa wananchi na aliwaahidi mambo mengi lakini hakuweza kuyafanya.

Unaambiwa katika video hiyo aliyoshare moja ya shairi linasikika likiimbwa “Napiga goti natubu kwa Mungu wangu na jamii nimefanya mambo mengi kwa kutumia cheo, naamini cheo dhamana, nisamehe nisamehe, nang’atuka nimeshaikosea jamii, nikajiita Mungu mtu nikajiita nabii, mwenyezi Mungu kumbuka nafasi hii napiga goti natubu daima nitakusihi, nangatuka nimeshaikosea jamii.

Hiyo ndiyo aliyoyaandika msanii huyo na kushare hisia zake kwa watu, msomaji wetu dondosha comment yako nasi tutaisoma na kuifanyika kazi.






Comments 1


  • Awesome Image
    Farajaemmanuel

    Naaminiii professor jay katka upigaji kazii hasa katka Sanaa unaweza big up sna mkuu

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags