Profesa Jay arudi rasmi kwenye siasa

Profesa Jay arudi rasmi kwenye siasa

Mwanasiasa Joseph Haule maarufu ‘Profesa Jay’ jana Jumatano Novemba 20, 2024 amerudi rasmi katika siasa baada ya ukimya wa muda mrefu uliotokana na kuugua.

Profesa Jay ambaye alikuwa mbunge wa Mikumi kwa kipindi cha 2015 -2020, jana kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha video ikimuonyesha akihutubia ikiwa na na ujumbe;

“Leo (jana) tumezindua kampeni zetu za uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye Kata ya Mikumi na Ruaha. Leo moto umeungua na maji yameloana, mpaka kieleweke,” ameandika.

Mbali na kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii pia Profesa Jay amewahi kutamba na ngoma kama Zali la Mentali, Kamili Gado, Utanambia nini, Kikao cha Dharura na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags