Producer Yogo Beats atangaza kuacha muziki

Producer Yogo Beats atangaza kuacha muziki

Mtayarishaji wa muziki nchini, Yogo Beats ametangaza kuachana na muziki kwa sasa kwa sababu ambazo bado hajaziweka hadharani.

Kupitia ukurasa rasmi wa Yogo Beats ameweka taarifa ya kutangaza rasmi kuachana na kazi hiyo ambayo inatambulika zaidi kama mtayarishaji wa muziki.

Kupitia posti aliyoweka ameandika “I quit the game, sitaki tena muziki, F **K This game” akisindikiza ujumbe huo ambao upo kwenye maandishi meupe na meusi kwa caption inayosomek kuwa – Too Much Hunting.

 Mastaa kibao wa muziki wameshangazwa na uamuzi huo huku wengi wamemuandikia kuwa aache utani na alichokiandika lakini wapo walianza kuuliza sababu ya kufanya hivyo ni nini.

Pia wapo walioshangazwa na taarifa hiyo wakiwemo mashabiki zake ambao wamemiminika kwenye comment wakitaka afute na kuacha kuweka hizo habari.

Itakumbukwa kuwa Yogo Beats anafanya kazi na mastaa kibao wa muziki hapa nchini aikiwemo Alikiba, ambaye amefanya naye kazi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags