Producer Geof Master afariki dunia, Roma amlilia

Producer Geof Master afariki dunia, Roma amlilia

Producer wa muziki nchini Geof Master ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye studio ya Tongwe Records amefariki dunia leo saa nne asubuhi kwenye Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

Akizungumza na Mwananchi mdogo wa marehemu Hollad Batista, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa chanzo cha umauti wa Geof ni Saratani ya kichwa.

Hollad amesema, Novemba mwaka jana Geof alianza kusumbulia na uvimbe puani na kisha akafanyiwa upasuaji kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini baada ya wiki tatu hali yake ilibadilika, uvimbe ukazidi ndani na nje ya pua.

Anasema baada ya hali hiyo, Januari 16 walimrudisha tena kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako walimhamisha kwenda Ocean Road ambako ndiko waliambiwa ndugu yao ana saratani ndani ya kichwa.

Kwa mujibu wa Holland msiba upo Tegeta jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika Jumatatu jioni saa 10, katika Makaburi ya Tegeta Wazo.

"Msiba upo Tegeta tunaendelea na taratibu nyingine, lakini mazishi yatakuwa siku ya Jumatatu kwenye Makaburi ya Wazo."

Geof alifanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki wa hip-hop nchini Roma Mkatoliki ambaye muda mchache uliopita ameposti picha kwenye mtandao wa Instagram na kuandika: "Nimempoteza kaka yangu, pacha wangu, rafiki yangu producer wangu (Tongwe Records), Rest in Peace Geaf Master, PUMZIKA MSUMULE."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags