Priyanka Chopra ampongeza mumewe kwa kumlea binti yao

Priyanka Chopra ampongeza mumewe kwa kumlea binti yao

Mwigizaji kutoka nchini India, #PriyankaChopra amempa pongezi mumewe #NickJonas na watu wengine walioshiriki kumlea binti yake Malti kwa wakati alipiokuwa katika kazi yake ya sanaa.

Tovuti ya The People News imeeleza kuwa mwigizaji huyo weekend hii ame-share picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na familia yake baada ya kutoka kuigiza nchini Australia na kutoa pongezi kwa watu waliyo mlea binti yake akiwemo mumewe.

“Hakuna kitu kama familia, mume wangu na marafiki kukufanya upate nguvu mpya kwa kunitunzia malaika wangu” ameandika.

Mwigizaji huyo, mwenye umri wa miaka  41, siku chache zilizopita alionekana Australia ana ‘rekodi’ filamu  ya ‘The Bluff’ ambayo iko katika hatua za mwisho kutoka, kulingana na maelezo yake baada ya ku-share picha mtandaoni.

Ikumbukwe kuwa Chopra na Jonas walifunga ndoa ya Kikristo mwaka 2018 katika Jumba la Umaid Bhawan nchini humo na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags