Post Malone ataja sababu ya kuchora tattoo usoni

Post Malone ataja sababu ya kuchora tattoo usoni

Rapa maarufu kutoka nchini Marekani #PostMalone amefunguka sababu ya kuchora tattoo usoni akidai kuwa alikuwa anatafuta mwonekano mzuri wa uso wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail News imeeleza kuwa Malone alifanya hivyo kwa kuwa alijiona hana mvuto hivyo tattoo hizo zimempa mvuto usoni.

 Post Malone hajawahi kuzifuta tattoo hizo ambazo zipo 14 usoni kwake huku akikaririwa mara kadhaa kuwa ana mpango wa kuziongeza.

Rapa huyo amewahi kufanya nyimbo mbalimbali kama vile: Sun Flower, Better Now, Wow, I like You, I Fall Apart, Rock Star, Congratulation na Goodbye.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags