Polisi: Mwenye taarifa sahihi kifo cha Zuchy azilete

Polisi: Mwenye taarifa sahihi kifo cha Zuchy azilete

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewataka watu wenye taarifa tofauti juu ya ajali ya bodaboda iliyotokea alfajiri ya jana Ijumaa Aprili 26, 2024, eneo la Makonde, mkoani Dar es Salaam na kusababisha kifo cha Noel Mwingira, maarufu Zuchy wazipeleke zifanyiwe kazi.

Katika ajali hiyo dereva bodaboda ambaye jina bado halijafahamika alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini ambapo kumeibuka mijadala mitandaoni ikiwemo lawama kwa Jeshi la Polisi ikidaiwa kuwa lilichelewa kufika eneo la tukio kutoa msaada licha ya wananchi kuwapigia polisi kwa ajili ya msaada waliishia kujibia kuwa gali halina mafuta.

Kutokana na mjadala huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime jana Ijumaa Aprili 26, 2024 ametoa taarifa kwa umma kuhusu tukio hilo akianza kwa kusema: “Kwanza, Jeshi la Polisi linasema hili ni tukio la huzuni na la kusikitisha kwa sababu tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika ajali hiyo.”

Katika taarifa hiyo Misime amesema tukio hilo liliripotiwa saa 10:12 alfajiri kuwa kuna ajali imetokea eneo la Mbezi Makonde. Baada ya kupokelewa taarifa hiyo  maofisa na askari waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa Tamasha la Shangwe la Utawala, lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers waliondoka wakiwa na gari ya Polisi  kuelekea eneo la tukio.

Amesema baada ya kufika waliuchukua mwili na kuupeleka Hospitali yaRufaa ya Mwananyamala kwa taratibu nyingine za kisheria.

Hivyo amewataka wanachi wenye taarifa sahii kuhusu ajali hiyo ambazo sio za ungo wazifikishe polisi ili zifanyiwe kazi na hatua za kisheria zichukuliwe.

“Endapo kuna mwenye taarifa tofauti na si za uzushi/uwongo kama hizo zinazosambazwa azifikishe kwa viongozi ili zifanyiwe kazi na hatua zichukuliwe.” Alisema Misime

Taarifa ambazo Mwananchi Digital limezipata, msiba wa Zuchy upo Chanika, jijini Dar es Salaam na taratibu za mazishi zinaendelea.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags