Pogba hatiani kufungiwa ‘soka’ miaka 4

Pogba hatiani kufungiwa ‘soka’ miaka 4

Mwanasoka nguli kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba yupo hatiani kufungiwa kucheza mpira miaka minne kwa kosa linaloelezwa kuwa ni utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku za kusisimua misuli.

Hii inakuja baada ya kufanyiwa vipimo mara ya pili na kubainika alitumia dawa za kusisimua misuli ambapo awali September 11 mwaka huu alisimamishwa kwa muda na mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Utumiaji wa Dawa za Kulevya ambapo aliomba uchunguzi huo ufanyike tena kwa mara ya pili.

Baada ya vipimo vya mara ya pili kugundulika kutumia madawa hayo atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka minne ambapo kuna uwezekano wa kupunguziwa nusu iwapo atathibitisha kuwa hakutumia dawa hizo kwa makusudi.

Huku mchezaji huyo akipewa siku saba za kuwasilisha utetezi wake kwenye mahakama hiyo kabla ya kutekeleza adhabu hiyo.

Ikumbukwe kutokana na sakata hilo ‘klabu’ ya Juventus imemsimamisha mchezaji huyo kufanya mazoezi na ‘timu’ hiyo huku ikisitisha mshahara wake kwa mwaka hadi 2026






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags