Pogba anukia Saudi Arabia

Pogba anukia Saudi Arabia

Mchezaji  Kiungo wa ‘klabu’ ya  Juventus, Paul Pogba  inadaiwa ni miongoni mwa nyota  wanaowindwa na ‘klabu’ za nchini Saudi Arabia,  Al-Ahli na Al-Ittihad ambazo zinatarajiwa kutuma wawakilishi wao muda wowote kuanzia sasa kwenda nchini Italy kwa ajili ya mazungumzo na wakala wa Pogba na wawakilishi  wa ‘timu’ ya Juventus ili kuona kama wanaweza kumpata mchezaji huyo.

Kama kawaida yao ‘timu’ hizo mbili zimekuwa zikichuana kwa kuchukua wachezaji wakubwa duniani kwa ajili ya ushindani katika ‘Ligi’ ya Saudia na haijajulikana dau la nani litamteka mchezaji huyo

Licha ya fundi huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ana mkataba hadi mwaka 2026. Hivi karibuni Pogba amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags