Pisi kali zinataka nini

Pisi kali zinataka nini

Yaani hazieleweki zinataka nini au zinataka mwanaume wa aina gani.

Mambo ya siksi paki, sijui urefu, sijui ujentlomani, sijui manini nini sijui.

Tunawaka rasmi sasa msimamieni kwenye suala moja tu la pesa. Kwamba pesa ndiyo msingi wa penzi penzini, mahaba habani, huba hubani na ulaazizi. Nau deizi hakunaga mapenzi ya kweli, ila pesa inaleta hisia za kweli.

Yaani meseji ya miamala ya pesa inawavutia zaidi kuliko tukio la kuvishwa pete. Ndo maana kizee kinaitwa baby na kinajidekesha na makunyazi yake usoni

Kwa sababu ndiyo mwezi ambao pesa zinahitajika zaidi kuliko ibada. Vibabu vinamiliki totozi kali kuliko mabishoo kwa sababu havina mkono wa birika…

Sasa we lamba lipsi na kuvimbisha kifua utaishia kuwa baunsa wa Konde Boy…
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post