Pisi kali hana pigo hizi

Pisi kali hana pigo hizi

Pisi Kali hanywi pombe kali wala ngumu. Anakunywa pombe laini tena zisizozidi chupa tatu kwa wikiendi tu. Siku za kawaida pisi kali hagusi pombe wala hana outing. Pisi kali akiitwa sehemu anaenda peke yake bila mashosti. Analipia usafiri mwenyewe na akikuta washikaji mezani, anawasalimia kwa lugha ya Joe Biden (Hi!).

Pisi kali hana namba ya bodaboda wala bajaji, hawajui wauza chips wala madalali wa vyumba.Pisi kali hajawahi kuona kandambili zilizokatwa mbele wala kusikia harufu ya visabuni vya guest. Pisi kali hajui neno tuma na ya kutolea.

Pisi kali ana namba chache kwenye simu, na zote zinajulikana na familia yake. Pisi kali hajui nauli sahihi ya mabasi ya mwendokasi. Pisi kali huona kitu cha ajabu sana mtu kuuza dawa ya mba, upele, mapunye, sumu ya panya.

Hivi ni vitu vigeni kwake. Mapunye? Upele? Mba? halafu hiyo sumu ataenda kuulia wapi hao panya? Pisi kali hajui kama panya wanaishi kwenye majumba ya watu mitaani. Picha linaanza pisi kali hajui hata maana ya neno kudanga.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags