Piga mishe hizi kuingiza kipato

Piga mishe hizi kuingiza kipato

Hatupoi, hatuboi mwanzo mwisho tunapeana vitu, Siyo kila mtu atabahatika kuajiriwa katika kampuni kubwa, na ndiyo maana kila mja na riziki yake, sasa watu wangu wa nguvu leo nimekuja kwenu kuwajuza mambo ambayo mnaweza kufanya na kuwaingizia kipato.
Katika Dunia ya sasa tumekariri kuwa mtu kufanya kazi kwenye kampuni kubwa ndiyo kuishi maisha mazuri lakini wanasahau kuwa vipo vitu vya kufanya ambavyo vinaweza kumfanya atoboe kimaisha.

Leo katika segment ya kazi tunaendelea tulipo ishia wiki iliyopita, baada ya kuandika baadhi ya kazi ambazo unaweza kuzifanya kwa kujiajiri wiki hii nimekushushia biashara ambazo unaweza kuzigeuza kuwa kazi na zikakupa jina kuliko hata unavyo fikiria.
Siku hizi kuwa na jina mjini ndiyo kila kitu na hizi ni baadhi ya kazi ambazo zinaweza kukupa jina (Umaarufu) na kurahisisha maisha yako kwa ujumla.



 Kufundisha
Moja ya kazi ambayo vijana wengi wanaidharau ni hii ya kufundisha lakini, ukiichukulia kwa ukubwa na kuikuza katika mitandao ya kijamii basi inaweza kukufanya ukawa mwalimu mkubwa nchini. Mfano mzuri kuna mwalimu ana-trend sana kupitia mitandao ya kijamii kutokana na kuibadirisha elimu kutoka kuwa ngumu na kuirahisisha.
Ambapo kufuatiwa na hayo imemrahisishia yeye maisha kwa kupata matangazo kutoka kwenye chapa mbalimbali. Ukiachilia mbali na hilo zipo day care nyingi zimefunguliwa omba kazi uingie mzigoni acha kufikiria kelele za watoto nenda kaipambanie kesho yako.

 Kupika kwa Oda
Wakati mimi niko chuo nilikuwa nafanya biashara ya kupika biriani kila Ijumaa kwa oda baadhi ya watu walinichukulia powa sana wakaona najivika utuuzima lakini wasichojua ni kuwa nilikuwa najiandaa na maisha mengine.

So kwako wewe ndugu uliye nyumbani unayesubiria kuajiriwa chukua hatua mapema unaweza, zunguka katika maofisi, kampuni chukua oda na uanze kupika hata kwenye masoko, kuzunguka kujitafutia riziki yako mwenyewe ni bora kuliko kukaa nyumbani kusubiri Mama/Baba arudi nyumbani umuombe pesa ya vocha, sabuni na mafuta.

 Kupiga picha
Moja ya kazi ambayo imekuwa ikiwaendeshea maisha baadhi ya vijana ni hii ya kupiga picha, karne ya sasa watu wamekuwa wakipenda sana kupiga picha kwa ajili ya kuacha kumbukumbu mbalimbali duniani so unaweza kuichukua hii na kuifanya kuwa kazi yako ya kudumu.

Tumia mitandao yako ya kijamii kukuza brand yako, tafuta watu ambao ni wakali au shule ambazo zinafundisha kozi fupi kasome ukimaliza rudi mtaani, ukishampiga picha mteja mmoja na picha ikawa kali basi bila kutumia nguvu utaona kila siku unajaliwa na wateja.


 Makeup Artist na kukodisha nguo za harusi
Wooooiii! Moja ya biashara au kazi ninayoitamani kila siku ni hii, sijui wenzangu mnaona ninacho kiona mimi au, niwaoneshe watu wangu wa nguvu, sasa ni hivi kila siku watu wanaolewa, kila siku watu wanapaka makeup kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe mbalimbali.


Wewe binti unayehangaika kutafuta kazi kwa nini usiende kujifunza jinsi ya kupaka Makeup, hii ni kazi ambayo kwa mtu mmoja hukosi 50k tuchukulie kwa siku umepata watu 5 upo wapi ndugu yangu, acha kukaa kizembe na kuzitazama fursa tu kwa wengine.

Tafuta mtu ambaye anaduka la kukodisha nguo za maharusi muombe uwe unatumia duka la nguo zake kutangaza kupitia mitandao yako ya kijamii naamini ukionesha kazi nzuri haweza kushindwa kukukajiri, kazi za siku hizi zinataka ujitoe ufahamu.
Na hii siyo kwa wanawake tu wapo wanaume mbalimbali wamekuwa wakifanya kazi za saloon kupamba maharusi, kwa nini wewe Mwanaume wa Kitanzania ushindwe acha kufikiria watu watazungumza nini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags