Picha ya chris Brown na Kehlani yazua gumzo mitandaoni

Picha ya chris Brown na Kehlani yazua gumzo mitandaoni

Mwanamuziki Chris Brown na msanii mwenzie Kehlan wamezua gumzo mitandaoni baada ya kuposti picha wakiwa pamoja ambayo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Chris Brown ame-share picha akiwa na Kehlan picha iliyopigwa Backstage kwenye moja ya show ya Breezy ya ‘11:11’.



Aidha picha hiyo ilizua gumzo mitandaoni huku baadhi ya mashabiki na wadau wakidai kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ambayo yameanza hivi karibuni, na wengine wakiweka wazi kuwa huenda Breezy na Kehlani wanatarajia kutoa ngoma.

Kufiatia na picha hiyo iliyoandikwa ‘Twin’ imezua hisia tofauti kwa mashabiki kutokana na wawili hao kutokuwa kwenye maelewano mazuri hapo zamani.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2016 Kelhani alijaribu kujiua ambapo Breezy aliibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumtolea maneno machafu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags