Peter Obi aishinda Lagos matokeo ya awali ya uchaguzi, Nigeria

Peter Obi aishinda Lagos matokeo ya awali ya uchaguzi, Nigeria

Peter Obi mgombea wa chama cha Labour amemshinda Bola Tinubu wa chama tawala katika eneo alilotoka, matokeo yaliyotangazwa na maafisa wa uchaguzi wa majimbo.

Mgombea urais wa chama cha tatu kwa ukubwa nchini Nigeria alisababisha ushindani mkali ambao ulizua ghadhabu kubwa kwa kushinda katika jiji kubwa zaidi la Lagos.

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1999 kwa chama hicho kinachoungwa mkono na  Tinubu, gavana wa Lagos mara mbili, kutoshinda jimbo hilo.

Aidha Tinubu ameshinda majimbo matatu kati ya matano yaliyotangazwa kufikia sasa.

Zaidi ya watu milioni 87 walistahili kushiriki katika uchaguzi huo, na kulifanya zoezi kuwa kubwa zaidi katika taifa la kidemokrasia zaidi barani Afrika.

Chama tawala cha All Progressives Congress (APC) na PDP vimetawala Nigeria tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999 lakini kwa sasa, Obi kutoka chama kisichojulikana sana cha Labour anatarajiwa kuleta upinzani mkubwa katika mfumo wa vyama viwili.

Peter anaungwa mkono na vijana wengi, ambao ni theluthi moja ya wapiga kura waliojiandikisha.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags