Pesa zilifanya Omah Lay aachane na mawazo ya kubadili dini

Pesa zilifanya Omah Lay aachane na mawazo ya kubadili dini

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Omah Lay ameweka wazi kuwa amewahi kufikiria kubadilisha dini kutoka katika Ukristo na kuwa Muislam.

Msanii huyo ameeleza hayo kufuatia mahojiano yake na mwandishi wa habari Wunmi Bello, Omah alifichua suala hilo la kufikiria kubadilisha dini licha ya kuzaliwa na kukulia katika familia ya kikristo.

“Nilitumia muda mwingi kanisani, na wakati fulani nilifikiria kubadili dini Lakini sasa niko katika hatua ambayo ni mimi tu na Mungu na siYo dini”

Katika mahojiano hayo Omah ameeleza kuwa mara tu baada ya kupata pesa alibadilika na kuanza kumuamini Mungu hivyo basi kwa sasa hajali kuhusu dini.

Stanley Omah Didia, maarufu kama Omah Lay, amejulikana zaidi kupitia nyimbo zake kama ‘Godly’ ‘Damn’ , ‘Reason’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags