Penzi la Lupita na Selema lafika ukingoni

Penzi la Lupita na Selema lafika ukingoni

Muigizaji kutoka nchini Kenya Lupita Nyong’o ameweka wazi kuwa ameachana na mpenzi wake Selema huku sababu ikiwa ni udanganyifu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lupita amethibitisha hayo kwa kueleza kuwa amechoka kuliweka suala hilo moyoni na kuficha ukweli unao muumiza.

Aidha ameeleza kuwa ameweka wazi suala hilo ili iwe fundisho kwa wengine wanaoumizwa na mapenzi kama yeye  na kutaka watu waache kumuhusisha na mtu mbaye hawezi kumuamini tena.

Ikumbukwe tuu Lupita na Selama waliweka wazi mahusiano yao kupitia mitandao ya kijamii mwishoni mwa mwaka 2022.

Lupita ameweza kuonekana katika movie mbali mbali ikiwemo Black Panther Wakanda Forever, Queen of Katwe, Little Monster nk.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags