peng shuai na sakata la ubakaji

peng shuai na sakata la ubakaji

Nyota wa Tennis kutoka nchini China, Peng Shuai amezidi kusisitiza kuwa watu hawakumuelewa kwa kiasi kikubwa katika chapisho lake kwenye mtandao wa Weibo kuhusu tamko lake la kulazimishwa kuingia katika mahusiano ya mapenzi na kiongozi wa zamani wa chama cha Chinese party.

Peng alichapisha andiko lenye maneno 1600 Novemba 2, 2021 katika ukurasa wake wa wa mtandao wa Weibo akimshutumu kiongozi wa ngazi ya juu wa zamani wa serikali ya China, Zhang Gaoli kwamba alikuwa anamlazimisha kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi bila ya ridhaa yake, andiko ambalo alilifuta muda mchache baadaye.

Na baada ya Peng kuandika tuhuma hizo hakuonekana kabisa kwa muda wa wiki kadhaa na kuleta hali ya sintofahamu katika jamii ya wanamichezo duniani.

Hii sasa ni mara ya pili Peng kufanya mahojiano na kukanusha tuhuma hizo akisema watu wengi walielewa vibaya kuhusu chapisho lake hilo na hakuna haja ya kuzidi kulizungumzia tena jambo hilo, huku wadau wengi wakichukulia kanusho hili kama propaganda ya kulimaliza sakata hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags