Pele apumzishwa katika nyumba yake ya milele

Pele apumzishwa katika nyumba yake ya milele

Mwanasoka nguli wa Brazil Pele ambae alifanya vizuri sana katika kucheza kwake mpira wa miguu, alipumzishwa katika nyumba yake ya milele baada ya zaidi ya  waombolezaji 230,000 kujitokeza na kuuaga mwili wake.

Kabla ya msafara wa mazishi kuanza, jeneza la mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia liliwekwa katikati mwa uwanja wa klabu ya Santos kwa masaa 24 ili aweze kuagwa.

Rais mpya aliyeapishwa hivi karibuni nchini Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alikuwa miongoni mwa watu waliofika uwanjani hapo, Ibada ya mazishi ilifanyika katika uwanja wa Vila Belmiro jana kabla ya jeneza jeusi la Pele kupitishwa katika mitaa ya Santos kwenye gari la zimamoto.

Hatimaye alizikwa huku bendi ikipiga muziki rasmi wa klabu ya Santos, Pele aliiongoza Brazil kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia  mwaka wa 1958, 1962 na 1970. Alifariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua saratani ya utumbo na matatizo ya moyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags