Pape Sakho Alivyojitabiria ushindi Tuzo ya CAF

Pape Sakho Alivyojitabiria ushindi Tuzo ya CAF

Oyaaaaweeeeh! Wale wanangu wa Simba kama nawaona vile ile furaha mlio nayo siku ya leo, kataka zilizo trend  bwana ni kuhusiana na mchezaji wa Club ya Simba mzee wa kunyunyiza, “Pape Sakho” kushinda tuzo ya bao bora Africa usiku wa kuamkia leo.

Lakini je? Ulijua kuwa mchezaji huyo alijitaaribia ushindi dakika chache tu kabla ya tuzo hizo? YES! Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sakho alipost picha na kuandika, “Are you ready to receive rthe trophy?” akimaanisha, “Mpo tayari kupokea kombe?” Mungu si Athumani wala Rama, akashinda kweli bhana!

Tuzo hizo za Shirikisho la soka Africa (CAF) ambazo zilitolewa jana usiku katika nchi ya Morocco, ambapo winga huyo wa Simba aliibuka kidedea baada ya bao alilofunga dhidi ya ASEC Mimosas kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) kunyakua tuzo ya bao bora Afrika, akiwapiku Gabadinho Mhango na Zouhair El Moutaraji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags