Papa mstaafu Benedict XVI kuzikwa leo Vatican

Papa mstaafu Benedict XVI kuzikwa leo Vatican

Papa Francis ataongoza leo ibada ya mazishi ya mtangulizi wake Benedict XVI mjini Vatican, Ni tukio ambalo halijawahi kushuhudiwa katika enzi za kisasa na linatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu.

Ikiwa ni karibu muongo mmoja baada ya Benedict kuwa papa wa kwanza katika karne sita kujiuzulu, mrithi wake ataongoza misa ya wafu katika uwanja mkubwa wa Kanisa la Mtakafitu Petro kabla ya mwili wake kuzikwa katika makaburi ya mapapa chini ya kanisa hilo.

Papa huyo mstaafu Mjerumani hakuwa kiongozi wa taifa lakini viongozi wa ulimwengu akiwemo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz watahudhuria mazishi hayo, pamoja na wafalme wa Ulaya na mapadre 3,700 kwa mujibu wa Vatican. Benedict, ambaye jina la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger, alifariki dunua Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags