Panya washindwa kulala kwa kukosa kujamiiana

Panya washindwa kulala kwa kukosa kujamiiana

Wanyama aina ya panya wa msituni wanaofahamika kama quolls, waliomo katika hatari ya kutoweka wanashindwa kulala kwa ajili ya kufanya ngono zaidi  na huenda hili linaweza kuwauwa, kulingana na utafiti mpya kutoka Australia.

Utafiti huo umebaini kwamba panya hawa wa kiume ambao husafiri mara kwa mara mbali kuwasaka wenza, katika maeneo ya mbali, mara nyingi hawasinzii wanapokuwa katika mchakato huo.

Ukosefu wa kupumzika unaweza kuelezea ni kwanini wanyama hawa wa kiume  hufa katika msimu mmoja wa kuzaliana , wataalamu wanasema.

Kwa upande mwingine wenzao wa kike wanaweza kuishi na kuzaa hadi miaka minne.

"Wanakwenda mwendo mrefu kujamiiana mara kwa mara na inaonekana kwamba hamu yao ni kubwa kiasi kwamba wanashindwa kulala na kutumia muda mwingi kuwatafuta quolls wa kike ," alisema Christofer Clemente, mhadhiriwa ngazi ya juu katika Chuo Kikuu cha Sunshine Coast.

Utafiti huo uliongozwa na Taasisi ya Christofer huku wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Queensland ambapo ulichapishwa jana Jumatano.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post