P Diddy alimpigia simu kaka yake Tupac, Kukanusha uvumi

P Diddy alimpigia simu kaka yake Tupac, Kukanusha uvumi

Mopreme ambaye ni kaka wa marehemu Tupac, ameweka wazi kuwa mwanamuziki P Diddy aliwahi kumpigia simu na kumueleza kuwa hakuhusika na kifo cha Tupac, licha ya baadhi ya wasanii akiwemo 50 Cent kushinikiza uvumi huo.

Kufuatia mahojiano yake jana Jumatatu na ‘Art of Dialogue’ kaka wa Tupac alieleza kuwa mwaka 2000 alipokea simu kutoka kwa Diddy ikimueleza kuwa yeye hakuhusika na mauaji ya mdogo wake ambayo yalitokea jijini Los Angeles.

Aidha Mopreme amekiri kuwa kupata majibu juu ya kifo cha Tupac imekuwa ngumu, na hajui nini cha kufanya kuhusiana na simu ya Diddy ingawa msanii huyo alitajwa na mshukiwa Keefe kuwa anahusika na mauaji hayo.

Tupac alifariki dunia mwaka 1996, kwa kupigwa risasi jijini Los Angeles.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags