Ozil asifia kiwango cha Maguire na Onana

Ozil asifia kiwango cha Maguire na Onana

Mchezaji wa zamani wa ‘klabu’ ya Arsenal, Mesut Ozil, amewapa maua yao wachezaji wawili kutoka ‘timu’ ya Manchester United, mlinda mlango Andre Onana, na beki Harry Maguire baada ya kuonesha kiwango kizuri kufuatia mchezo wa jana ‘Ligi’ ya mabingwa Ulaya.

Ozil ametoa sifa hizo baada ya siku za hivi karibuni Onana na Maguire kukosolewa kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kutoisaidia ‘timu’ ya Man United kupata matokeo mazuri.

Kupitia ukurasa wake wa X wa Ozil ameandika ujumbe usemao “Harry Maguire na Andre Onana wamestahili hilo, wamewanyamazisha waliokuwa wanawachukia”

Maguire na Onana waliupiga mwingi kufuatia mchezo wao na Copenhagen FC uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford na kuondoka na ushindi wa bao 1-0 huku Migaire akitupia bao pekee na Onana kuokoa 'penati' dakika za mwishoni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags