Orodha ya ngoma za Diddy yazidi kushuka

Orodha ya ngoma za Diddy yazidi kushuka

Orodha ya muziki pamoja na ngoma za Diddy imeripotiwa kushuka kwa kiasi kikubwa kwenye redio, hii ni baada ya kuhusishwa kwenye biashara za ngono.

Kushuka kwa uchezwaji wa ngoma hizo redioni kumeripotiwa kuanza toka mwezi Novemba mwaka jana wakati Diddy alipofunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono na aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

Kwa mujibu wa Billboard imeeleza kuwa toka Cassie afungue kesi mahakamani ngoma za Combs zimekuwa zikishuka katika upande wa wasikilizaji na watazamaji ambapo, awali ilizoeleka kuwa nyimbo zake zilikuwa zikifuatiliwa na zaidi ya watu milioni 23.3 lakini sasa ngoma hizo zimeshuka mpaka wafuatiliaji milioni 4 tu.

Uporomokaji huo wa muziki kwa Diddy umeripotiwa kushuka kwa asilimia 88 kwenye uchezwaji redioni na kushuka kwa asilimia 83 kwa wasikilizaji redioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags