Ommy: Diamond akiwa tajiri namba moja msiniite chawa

Ommy: Diamond akiwa tajiri namba moja msiniite chawa

Mwanamuziki Ommy Dimpoz amewataka mashabiki na wadau mbalimbali kutomuita chawa endapo Diamond atapokuwa tajiri namba moja duniani.

Kutokana na video ya Diamond iliyosambaa juzi Septemba 3 akieleza ndoto yake ni kuwa tajiri namba moja duniani Dimpoz amejibu kwa kuchapisha picha wakiwa pamoja huku akiwaasa Watanzania kutomuita chawa kwani yeye na Simba wametoka mbali.

“Jamani Watanzania nadhani mmeona line nimetoka nayo mbali sana ole wenu akiwa tajiri namba moja tukiwa tunakula piza kwenye private jet mniite chawa, na tajiri kaniahidi atanikopesha niinunue Yanga” amendika Dimpoz

Utakumbuka kuwa ndoto hiyo ya kuwa tajiri namba moja duniani Diamond aliisema wakati wa uzinduzi wa tamasha la Wasafi Festival

“Ndoto yangu kubwa katika maisha ni kuwa tajiri namba moja duniani, ndio ndoto yangu na ninakuthibitishia kwamba nitakuwa tajiri namba moja duniani. Kwa sababu kwangu mimi naamini kila kitu kinawezekana, na ninawahakikishia kuwa mtanzania nitakayewakilisha taifa kwa kuwa tajiri namba moja duniani” alisema Diamond



Ikumbukwe kuwa urafiki wa wawili hao ulianza kitambo tangu hawajatoboa kimaisha ambapo wakati wa harakati zao za kujitafuta walifanikiwa kushirikishwa katika ngoma ya Dully Sykes iitwayo ‘Utamu’ iliyotoka mwaka 2015 na ‘Prokoto’ wimbo waliyoshilikishwa na Victoria Kimani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags