Offset amshauri Cardi B kutoa album

Offset amshauri Cardi B kutoa album

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #Offset amemshawishi mama wa watoto wake #CardB kurudi studio kwa ajili ya kutoa albamu yake ya pili baada ya miaka 6 kupita.

Kwa mujibu wa TMZ News imeeleza kuwa msanii huyo ameonesha kumtia moyo na kum-support #CardiB kwa kuwaambia mashabiki wake nchini humo wakae mkao wa kula kwa ajili ya albamu mpya kutoka kwa mama watoto wake kwani anaamini kuwa Albumu hiyo itakuwa na ngoma kali zaidi.

Ikumbukwe kuwa albumu ya mwisho kutolewa na CardiB ilikuwa ya ‘Invasion of Privacy’ mwaka 2018 ambayo ndiyo ilikuwa album yake ya kwanza ikiwa na nyimbo 13, akiwashirikisha baadhi ya mastaa wakiwemo SZA, 21 Savage, Bad Bunny, J Balvin na wengineo.

Licha ya wawili hao kuendelea kuonekana pamoja huku mara ya mwisho ikiwa ni siku ya ‘Valentines Day’ lakini bado hawajaweka wazi kuhusu kurudiana kwao baada ya #Cardi kutangaza kuachana na aliyekuwa mumewe huyo mwishoni mwa mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags