OCS Mwakinyuke: Bila washauri wazuri kwenye sanaa unapotea

OCS Mwakinyuke: Bila washauri wazuri kwenye sanaa unapotea

Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata, OCS David Mwakinyuke amesema ni muhimu wasanii kupata mshauri mzuri na kutoingia katika vishawishi ili kulinda kipaji.

Mwakinyuke amezungumza jana Ijumaa Agosti 30, Tabata Dar es Salaam wakati anazindua Tuzo za Kipaji Awards.

"Jinsi unavyokuwa staa kwenye sanaa yako ndipo mikataba minono inakuja na shetani hakai mbali na wewe, kuanzia madawa ya kulevya na ulevi, kitachotokea kama usipokuwa na washauri wazuri sanaa yako na kipaji chako na ustaa wako havitakulipa kwa sababu utadhohofu kwa magojwa ya akili au mwili kutokana na miadalati au tutakuzika mapema kwa sababu kila binti mzuri au kaka mzuri utamtaka,"amesema

Amesema miaka ya nyuma hata yeye alikuwa akifanya sanaa lakini ndoto zake zilikatika kutokana na ushauri wa mama yake.

"Kipindi hicho na mimi naimba aliyefanya nisiendelee na usanii ni mama yangu alikuwa ananiogopesha sana alikuwa anasema ikitokea umeumwa utaweza kufanya shoo bahati mbaya kipindi hicho dunia ilikuwa haipo leo ambapo unaweza kufanya kazi zako zikabaki ukawa na copy right ambazo watu wakitumia unaweza kulipwa tulikuwa hatupo katika dunia ya kuangalia ya mbele, yale maneno yaliniingia nikaona niache"amesema

Hata hivyo kati ya wasanii walioibuka kidedea kwenye tuo hizo ni Dr Almas na Black Pass






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags