Nyumba iliyoigiziwa filamu ya Home Alone yauzwa

Nyumba iliyoigiziwa filamu ya Home Alone yauzwa

Nyumba maarufu iliyopo katika kitongoji cha Winnetka, Illinois Chicago ambayo ilitumika kuigizia filamu ya ‘Home Alone’ ya mwaka 1990 inauzwa.

Nyumba hiyo ambayo imewekwa katika tovuti za uuzaji wa bidhaa mbalimbali zisizo hamishika ya ‘Coldwell Banker Realty's Dawn McKenna Group’ imeripotiwa kugharimu kiasi cha dola 5.25 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 13.6 bilioni.

Aidha kwa mujibu wa tovuti ya ABC7 imeeleza kuwa mjengo huo wenye vyumba vitano, bafu sita, sehemu ya michezo, sehemu ya kutazama sinema nk. haitakuwa na muonekano kama wa hapo awali kwani wamiliki walibadilisha muonekano na kuweka wa kisasa zaidi.

Nyumba hiyo ilitumiwa na Kevin McCallister katika filamu ya Krismasi ya mwaka1990 ‘Home Alone’ ambayo iliongozwa na Chris Columbus.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags