Nyota wa Brookly nine–nine afariki dunia

Nyota wa Brookly nine–nine afariki dunia

Muigizaji maarufu kutoka nchini #Marekani, #AndreBraugher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Braugher aliwahi kuigiza tamthilia na filamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘Brooklyn Nine-Nine’, ‘Homicide’, ‘Life on the Street’, ‘Men of a Some Ag’e na ‘Glory’.

Braugher ambaye alizaliwa na kukulia Chicago, Marekani, alipata shahada ya kwanza ya sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Stanford na shahada ya uzamili ya sanaa kutoka Chuo cha Juilliard,  New York City.

Mwaka 1991, Braugher alifunga ndoa na muigizaji mwenziye #AmiBrabson, ambaye alikutana naye kwenye filamu ya ‘Homicide Life on the Street’ na wamefanikiwa kuwa na watoto watatu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags