Nyota wa Black Panther afariki dunia

Nyota wa Black Panther afariki dunia

Connie Chiume, mwigizaji mkongwe wa Afrika Kusini ambaye alionekana katika filamu ya Marvel Black Panther, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na familia yake, ikieleza kuwa jana Jumanne mchana Agosti 6, 2024 mwanamama huyo alifariki akiwa katika Hospitali ya Johannesburg alipokuwa akipatiwa matibabu huku sababu ya kifo chake ikiwa haijawekwa wazi.

Katika filamu ya Black Panther ya 2018, Chiume aliigiza kama Zawavari - Mwanachama wa Baraza la Kikabila la Wakanda, vilevile katika muendelezo wa 2022 Black Panther: Wakanda Forever alichukua nafasi ya Zuri (Forest Whitaker) kama Mzee Statesman wa Wakanda.

Aidha enzi za uhai wake Chiume alionekana katika filamu kama Rhythm City. Pia alionekana katika filamu ya muziki ya Beyoncé ya Disney iliyotokana na The Lion King, ambayo alicheza kama mama wa Simba, aitwaye Sarabi, Heart of the Hunter na filamu nyinginezo.

Kutokana umakini wake kwenye kuigiza amenyakua tuzo mbalimbali zikiwemo Tuzo ya NTVA Avanti ya Mwigizaji Bora wa Kike, Tuzo ya Filamu na Televisheni ya Afrika Kusini (SAFTA) ya Mwigizaji Bora msaidizi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags