Njia za kutosahau uliyosoma

Njia za kutosahau uliyosoma

Na Michael Onesha

Niaje niaje watu wangu wa Mwananchiscoop, naona harakati za chuo kama zimetaradadi, kama tunavyojua kipindi hichi ni kipindi ambacho baadhi ya vyuo vinafanya mitihani yaani University Examination (UE), na ndiyo wakati wa kuhaha wa baadhi ya wanafunzi wasiopenda kusoma.

Nami leo nimekuja na mbinu kabambe ambayo itakusaidia wewe mwanafunzi kusoma bila kusahau, kama waswahili wasemavyo, kichwa kina vitu vingi, lakini likifika suala la kukaa chini na kusoma basi inabidi usome kweli kweli.

Moja ya tatizo ambao linawasumbua wanafunzi wengi ni kusoma na kisha kusahau kile walichokisoma au kufundishwa. Kutokana na changamoto hiyo leo katika Unicorner tumeamua kukuletea njia mbalimbali za kusoma ambazo zitakusaidia na kukuwezesha usisahau wakati ukiwa unasoma.

  1. Penda unachosoma

Ukisoma kitu unachopenda kuna uwezekano mkubwa wa wewe kukumbuka, na ndiyo maana kabla hujachagua course unayosomea unatakiwa kuichunguza, je unaipenda na itakufaa?.

Jiulize ni nyimbo ngapi unaweza kuziimba, wala hukufanya bidii yoyote kuzikariri lakini zipo kichwani. Ni kwa sababu ulizipenda nyimbo hizo hivyo unaposoma penda kile unachosoma, soma ukitabasamu, usikunje sura, elimu siyo vita.

  1. Kuwa na malengo wakati wa kusoma

Unapoanza kusoma jiulize kwa nini ninasoma kitu hiki? ukiweza kujua kwa nini umeamua kusoma course hiyo au masomo uliyoyachangua basi huwezi kusahau hata kidogo na itakufanya ufahulu katika mitihani yako, najua kabisa wanafunzi wengi husoma kwa ajili ya mitihani hivyo basi cha kuzingatia ni wewe kutofeli soma hilo unalosoma maana ndiyo hatma ya maisha yako ya baadaye.

  1. Jipime mwenyewe unaposoma

Unaposoma kuwa na kalamu na daftari, baada ya kila kipengele jipime ili kuona kama unakumbuka, kwa mfano kama unasoma mada fulani hakikisha kila unapomaliza jikumbushie bila kuangalia kwenye daftari lako, kama unayakumbuka yote uliyoyasoma, hii itakusaidia sana haswa uwapo katika chumba cha mtihani ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kukumbuka yale yote ya muhimu uliyo yasoma.

 

  1. Rudia tena na tena

Ukirudia mara nyingi utakumbuka, hivyo basi usisome mara moja ukoana umemaliza, unapaswa kurudiarudi, pale unapofundishwa darasani isome mada hiyo, unapopata muda tena baadaye nenda usome tena na unapotangaziwa mtihani soma tena. Mada moja ukiirudia kuisoma mara saba kwa vipindi tofauti tofauti huwezi kuisahau.

  1. Fanyia mazoezi ulichokisoma

Njia hii ni bora na inasaidia kukumbuka kwa haraka zaidi, kuna njia mbili za kufanyia mazoezi kile ulichokisoma kwanza ni kumfundisha mtu kile ulichosoma. Soma kisha muite rafiki anza kumfundisha ulichosoma. Njia ya pili soma mada fulani kisha ita marafiki zako na muanze kujadiliana kwenye group lenu, na kama ni kipindi cha mitihani basi anza kwa kusoma peke yako kisha likiwa limebaki saa moja kabla ya mtihani tafuta group la watu muanze ku-discuss mliyosoma wote kwa pamoja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags